Thursday, 16 March 2017

WAPIGANA WAKIGOMBEA FEDHA YA SODA ILIYOTOLEWA NA RAIS MAGUFULI

Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Vikonje A wilayani Chamwino mkoani Dodoma wamezichapa kavukavu wakigombea TZS 100,000 iliyotolewa na Rais Dkt Magufuli wanunue soda.
Rais Dkt Magufuli alitoa fedha hizo kwa wakazi hao wa kijiji kilichopakana na Ikulu ndogo ya Chamwino aliposimama kuwasalimu wakati akiwa njiani kuelekea kwenye makazi yake.
_94888823_cola640
Mwenyekiti wa Kitongoji hicho alisema jana kuwa, alipopokea fedha hizo aliwapa wanaume 40,000 na wanawake kiasi hicho hico huku 20,000 akiielekeza kuchangia ujenzi wa shule ya msingi kijijini hapo. Kiongozi huyo alisema kuwa, ugomvi uliibuka upande wa wanaume ambao baadhi walitaka mgao mkubwa kuliko wengine.
Licha ya kuwa kiongozi huyo aligawa fedha hizo watu wakiona na kumpa Diwani 20,000 ya mchango wa shule, baadhi ya watu walimtuhumu kuwa amezichukua kwa ajili ya matumizi yake binafsi.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Kitongoji, Robert Mshana aliwataka wakazi wa Kijiji hicho kubadilika kwani eneo hilo litakuwa eneo muhimu kutokana na Ikulu ya nchi kuhamia hapo.
Mshana aliyasema hayo wakati wa kikao cha kijiji kilicholenga kuwaelimisha wanakijiji juu ya mipaka ya Ikulu ya Chamwino na kuorodhesha mali zao ili waweze kulipwa fidia kupisha upanuzi wa Ikulu.
-Mwananchi

from Blogger http://ift.tt/2m0okFQ
via IFTTT

from WordPress http://ift.tt/2mNUDXw
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2m0Qhxn
via IFTTT

from WordPress http://ift.tt/2mJAfVM
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2naVEKc
via IFTTT

from WordPress http://ift.tt/2mP9Ffi
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2nbL19V
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2mtS3m2
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2muggZh

No comments:

Post a Comment