Thursday 30 March 2017

Uzuri na ubaya wa ‘selfie stick’..

Kwa mtu yeyote anayependa kufuatilia masuala ya teknolojia lazima atakuwa anafahamu kuhusu kifaa kilichojipatia umaarufu mkubwa ndani ya muda mfupi sana tangu kujulikana kwake.
‘Selfie sticks’ au fimbo za kuwekuwezesha kujipiga picha kwa kutumia kamera ya mbele ni ukweli usiofichika kuwa zimetokea kupendwa na wengi sehemu nyingi duniani pamoja na watu maarufu duniani wametokea kuvutiwa na selfie stick.
Image result for selfie stick
Kila kitu kina faida na hasara zake ila uzuri/ubaya utatokana na wingi au uchache wa kitu fulani au jambo fulani. Pata kufahamu uzuri/ubaya wa selfie sticks:-
Uzuri/faida za selfie sticks.
a) Urahisi wa upigaji picha/uchukuaji wa picha jongefu (video). Ni wazi kwamba selfie sticks zimerahisisha sana wakati wa upigaji picha au uchuaji wa picha. Selfie stick inawezesha kuchukua picha nzuri bila kujali ukaribu au umbali wa mhusika/wahusika katika picha/video hiyo.
b) Urahisi wa kuitumia. Selfie stick haihitaji dakika 5 kuweza kujua jinsi ya kuitumia kwani ni rahisi sana kuitumia hivyo basi huhitaji kutumia fikra nyingi kuweza kujua namna ya kuitumia.
Kwa kubonyeza kitufe cha katikati basi utakuwa umeruhusu picha kupigwa.
c) Fursa katika biashara. Ujio wa selfie stick kwa kiasi fulani umeongeza kipato kwa wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara hiyo kuanzia yule anayezileta kutoka ughaibuni mpaka yule muuzaji wa rejareja.
d) Urahisi wa kuibebeba. Selfie stick inaweza ikaongezeka urefu na kupungua urefu kulingana na mahitaji lakini kubwa zaidi si nzito kabisa na inaweza kuwekwa katika mfuko wa suruali na mtu mwingine asijue kama mfukoni una selfie stick.
Ubaya/hasara za selfie sticks.
a) Gharama. Wakati selfie sticks zinafika hapa kwetu zilikuwa zikiuzwa kati ya Tsh. 35 elfu mpaka 40 elfu kiasi ambacho si watu wote wenye kumiliki simu wanaweza kununua kifaa hicho. Hata hivyo hivi sasa zimeshuka bei na kuuzwa kati ya elfu 25 mpaka 30 elfu.
b) Kutokuwa na faragha. Selfie sticks hazina usiri kwani hata kama ukiitumiaje picha zilizopigwa kwa kutumia selfie stick zinajulikana kwa haraka sana. Hii inaweza kuwa inasababishwa na kwamba utumiaji wa selfie stick umezoeleka sehemu nyingi duniani.
Ni wazi kuwa faragha kwenye picha zilizopigwa kwa kutumia selfie stick ni sawa na hakuna kitu kabisa.
c) Ulimbukeni. Kwa kiasi fulani selfie sticks zimeweza kuonyesha tabia ya mtu ilihali mwanzoni tabia hiyo haikujulikana. Kwa limbukeni wa selfie stick anaweza kutumia kifaa hicho katika sehemu zisizostahili mfano katika nyumba za ibada, msalani, n.k.
d) Uharibifu wa mali. Katika harakati za kuweza kupata picha/video nzuri mtumiaji asipokuwa makini anaweza akaharibu vitu vilivyopo karibu wakati wa kurefusha selfie stick.
Tazama video hii fupi kuweza kuamua mwenyewe iwapo selfie sticks ni mbaya au nzuri kisha tupe maoni yako.
Tazama video Mtoto amvua kofia Papa Francis

from Blogger http://ift.tt/2nlGy1a
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2nxZf2D

No comments:

Post a Comment