Saturday 25 February 2017

JINSI VITAMBI VINAVYOSABABISHA UGUMBA NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Watu wanaofurahia wameelezwa kuwa vina madhara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuumwa magoti, miguu na kupata matatizo ya moyo.
Madhara mengine ni kuharibika muonekano, tatizo la kusahau, kisukari cha ubongo (type 3 diabetes), shinikizo la damu, upungufu wa nguvu za kiume na ugumba.
Mtaalamu wa ushauri elimu ya mapishi na sayansi ya jikoni kwa watu wanaosumbuka na magonjwa mbalimbali ya lishe, Dkt. Boaz Mkumbo, amesema sukari nyingi mwilini kwa wanaume hupandisha homoni ya insulin inayovuruga homoni ya kiume (testosterone).
“Homoni hii (ya testosterone) inajenga misuli, kukupa nguvu na shauku ya ndoa kwa jinsia tofauti, inaposhuka chini ya kiwango husababisha kuongezeka kwa estrogen, homoni ambazo hupunguza maumbile ya sehemu za siri,” alisema.
Kwa mwanamke, wanga na sukari huwa inapandisha homoni hiyo ambayo ni askari wa sukari kwenye damu, kisha kuvuruga homoni zote zinazohusika na mfumo wa mzunguko wa kike. Dkt. Mkumbo amesema mtu akishaona dalili hizo lazima atambue kuwa mwili wake umeshaonesha dalili za kutostahimili kuendelea kutumia wanga na sukari.
“Kitambi ni hali inayosababishwa na vichocheo vinavyohusika kuunguza na kuhifadhi mafuta kutokuwa katika mihimili wake. Vikiwa vingi vitakuhifadhia mafuta mengi na vinasababisha mafuta yasiunguzwe. Visipokuwa katika mihimili wake, unapata kitambi,” alisema Dkt. Mkumbo.
Kuna homoni sita ambazo huendesha mwili wa binadamu na zote huhitaji kipimo sawasawa na matumizi yake, lakini homoni ya insulin ikizidiwa ndipo homoni zote huvurugika, ndipo mtu huanza kunenepa.
Mtaalamu wa lishe Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mariam Nyamwaira alisema katika wiki ya lishe Januari mwaka huu, ni Watanzania asilimia 10 pekee kati ya waliojitokeza kupima afya walionekana kuwa na afya sawa.

from Blogger http://ift.tt/2lFU4yk
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2lFU5k1

No comments:

Post a Comment