Tuesday 16 August 2016

WAMILIKI WA VIBANDA STENDI MAKAMBAKO WAHOFIA KUKUTWA NA YA MWANZA

WAFANYABIASHARA na wamiliki wa vibanda kuzunguka stendi ya Makambako,
wamepata hofu ya kufungiwa vibanda vyao baada ya halmashauri tya mji wa
Makambako mkoani Njombe  kuwapa taarifa
za kufanya uhakiki wa vibada vyote katika stendi hiyo.
Wafanyabiashara hao waliambiwa na halmashauri katika mkutano
wao na afisa biashara kuwa wanahitajika kufanyiwa uhakiki wa kila kibanda
katika stendi hiyo na kuwapa mkataba wa malipo ya kodi ya ardhi katika eneo
hilo.
Wakizungumza na afisa biashara wa halmashauri ya mji Makambako
wafanyabiashara hao walisema kuwa wanawasiwasi wa kuja kufungiwa vibanda vyao
baada ya uhakiki huo.
Chesco Ngweta alisema kuwa wanavyo jadili kuhusu mkataba
unaotarajiwa kuwekwa baina yao na halmashauri inawajia kumbukumbu ya kile
kilicho fanyika halmashauri za moja mkoani Mara.
Alisema kuwa serikali inatakuwa kuwatambua na mkataba huo upakapo
letwa kwao usainiwe baada ya kuupitia na kuuelewa.
Aidha afisa biashara Carros Mwenga alisema kuwa baada ya
uhakiki huo halmashauri inatarajia kuanza kujipatia ushuru wa ardhi na kuongeza
kwa vibanda ambavyo havija endelezwa vinandelezwa.
Alisema kupitia uhakiki huo vibanda hivyo vitatambuliwa
ambavyo vinawatu na ambavyo bado havina watu na kupatiwa watu kwaajili ya
kuviendeleza.
Alisema kuwa wafanyabiashara wakikubaliana kuto kubaliana
yaliyo tokea katika mikoa ya Mwanza na Mara yatatokea lakini wakikubaliana
kukubaliana hakuna atakaye fungiwa katika stendi hiyo.
Wamiliki hao wanawasiwasi wa kutokea yale yaliyo tokea Kwenye
stendi za mikoani ya Mwanza na Mara halmashauri kufunga baadhi ya vibanda.

from Blogger http://ift.tt/2bnSs56
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2bCIKQM

No comments:

Post a Comment