Tuesday 26 July 2016

Wafugaji njombe kuelimishwa ufugaji wa kisasa

WAFUGAJI wa ng’ombe wa mkoani Njombe wametakiwa kuongeza uzalishaji na ubora wa maziwa pamoja na kutumia vizuri maziwa kwa kunywa ili kuimarisha afya zao na familia zao kabla ya kuipeleka maziwa hayo kiwandani kitu kinacho sababisha familia zao kuwa na afya duni.
 
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya uwekezaji ya mfuko kichocheo wa SAGCOT, Dr Rosebud Kurwijila, wakati akizungumza na badhi ya wafugaji mkoa wa Njombe walio kwenye semina ya siku tano kwaajili ya kujifunza kuinua kipato chao kutokana na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa kibiashara na kuachana na ufugaji wa kawaida ambao hauwapatii faida na kipato cha kutosheleza.
 
Semina hiyo ni ya nne kutolewa Tanzania ambayo inatolewa na Mfuko Kichocheo wa SAGCOT kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara, (UNCTAD) ikilenga kuinua uchumi wa wafugali wa ng’ombe wa maziwa kwa kunufaika na kipato kikubwa kutokana na mazao ya Ng’ombe.
 
Kurwijila alisema kuwa mafunzo hayo ni kuhakikisha kuwa wafugaji wanaondokana na kulima kilimo cha kujikimu na kupata kipato cha kuendeleza maisha yao kwa uchumi unao tokana na kilimo biashara.
 
Alisema kuwa kuwa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT unatoa ufadhili kwa wafugaji hao kupitia Kiwanda cha kusindika maziwa cha Njombe ambapo Mfuko Kichocheo wa SAGCOT ilifanya utafiti wa kujua nini mfugaji anahitaji ili kuinuka kiuchumi.
 
Katibu Mtendaji wa Mfuko kichocheo wa SAGCOT John Kyaruzi amesema kuwa sasa ni wakati kwa wafugaji kuwa matajiri kutokana na ufugaji na ndio maana ufadhili wa kutolewa kwa elimu wafugaji ili kufuga kibiashara ambapo wafugaji katika mahitaji yao ni ng’ombe mweye uwezo wa kutoa maziwa kwa wingi.
Kyaruzi alisema kuwa wafugaji wengi katika hatua ya kulisha mifugo yao wapo vizuri lakini wanacho kikosa ni kupata ng’ombe wazuri wa maziwa na kuwa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT kamwe haita toa mkopo wa pesa kwa wakilima na kuwa itatoa uwezeshaji wa kilie mfugaji anacho hitaji ili kuinuka kiuchumi.
 
Alisema lengo la kutoa elimu hiyo ni kuinua mfugaji kufanya ufugaji kibiashara na kiuchumi na kuwasaidia wafugaji hao kuwainua kiuchumi hasa kwa ukanda wa juu kwa kuwa hapo awali wakulima walikuwa wakiwezeshwa kwa kuwapatia pesa lakini cha muhimu imegundulika ni elimu.
 
Aidha mkurugenzi wa halmashauri ya mji Njombe, Iluminata Mwenda alisema kuwa wafugaji hao watumie vizuru fulsa hiyo kwa kuwa wanaletewa elimu ya kuwa na uchumi mzuri na kuwa wafugaji wakifanya vizuri halmashauri nayo itaongeza kipato chake kwa kuwa kiwanda cha maziwa kitazalisha kwa wingi.
 

 
Mratubu wa biashara wa Mfuko Kichocheo SAGCOT, Abdala Msambachi   akitoa ekelimu kwa wagugaji wa ng’ombe wa maziwa mkoani Njombe ili kufanya ufugajiwa kisasa na uinua uchumiwao elimu hiyo inayo tolewa na Mfuko Kichocheo SAGCOT.

from Blogger http://ift.tt/2a2EaX4
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2a1fJZg

No comments:

Post a Comment