Friday 15 July 2016

MADAWATI YANATOSHEREZA NJOMBE

MKUU wa Mkoa wa Njombe DR. Rehema Nchimbi amewaagiza
wakurugenzi kutoa maeneo kwa waalimu kwaajili ya kila shule kuwa na miti ya
mipatachichi ili kuwapunguzia waalimu ukali wa maisha huku waalim hao
wakimpatia pesa kwaajili ya madawati ikiwa ni kuunga mkono juhudi ya Rais ya
kuhakikisha kuwa watoto hawakai chini.
DR. Nchimbi amewataka waalimu hao kuomba maeneo kwa
wakurugezi wa halmashauri ili waalimu hao kupanda miti ya miparachichi na
kusema kuwa katika shule zake hakuna wanafuzi wanao kaa chini na kusema kuwa
halmashauri pekee ya Ludewa ndio kunashida ya madawati licha ya kuwa vifaa
vyote vinavyo hitajika kuwepo.
Mkuu wa mkoa huyo amewaambia waalimu hao kuwa wajikite katika
ujasiliamali na kujikwamua na ugumu wa maisha huku pesa walizotoa kwaajili ya
madawati zilizotolewa na CWT kitengo cha wanawake na walemavu kurejeshwa kwao.
Walimu hao wamesema kuwa wanaunga mkono juhudi za Rais Dr.
John Magufuli, kuhakikisha wanafunzi hawakai chini kwa kuchangia shilingi laki
saba kwaajili ya kununua madawati.
Waalimu kitengo cha wanawake na walemavu mkoa wa Njombe wapo
katika semina ya kujengeana uwezo na mafunzo ya ujasiliamali ili kujikwamua na
matumizi mabaya ya pesa za mishahara.

from Blogger http://ift.tt/29AOmJI
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2a4epcE

No comments:

Post a Comment