Thursday 24 December 2015

Ndovu 145 zanaswa Dar


Picha na Maktaba,
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limekamata meno ya tembo 145 ambayo sawa na tembo 45.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mchana Jijini Dar es salaam,Kamishna wa Kanda ya Maalum ya Polisi,ACP Suleiman Kova amesema Mnamo tarehe 21/12/2015 Polisi walipata taarifa za  kuaminika kutoka kwa raia mwema kwamba maeneo yaTemeke Sudan kuna nyumba ambayo zinahifadhiwa nyaraza serikali,

Kamishna Kova ameendelea kusimulia akisema mara baada ya kupata taarifa hiyo upekuzi ulifanyika nyumbani kwa mtu anajulikana kwa jina la RAMADHANI S/O AYUBU MNEKEA, Miaka 55, Dereva, Mkazi wa mtaa wa Miburani, Temeke jijini Dar es Salaam,

Hata hivyo Kamishna kova amesema Taratibu zote za upekuzi zilifanyika na katika upekuzi huo Jeshi hilo walifanikiwa kugundua na kukamata vipande 156 vya meno ya Tembo.

Vilipomimwa Vipande hivyo kitaalam vinauzito wa kilo 211.66. aidha, vipande  hivyo ni sawa naTembo 45 waliouwa wanathamani yake katika soko haramu ni shilingi Bilioni moja na milioni mia nane za kitanzania.

Vilevile katika Ujangili huo jeshi linawashikilia watuhumiwa waliokutwa na nyara hizo ambao ni RAMADHANI S/O AYUBU MNEKEA, Miaka 55, Dereve, Mkazi wa Mtaa wa Miburani, Temeke Dar es Salaam

Mwengine ni  ROBERT S/O IZAK, Miaka 32, Fundi Ujenzi mkazi wa Mabibo jijini Dar es Salaam ambaye anatuhumiwa kwamba aliletamzigo huo kwamtuhumiwa wa kwanza RAMADHANI S/O AYUBU MNEKEA.


Katika hatua nyengine Jeshi la Polisi Kanda Maalumya Dar es Salaam linaendelea kuwahoji wafanyakazi wa idara mbalimbali wakiwemo wa MamlakayaBandari Tanzania (TPA), mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wamiliki na watumishiwa ICD’s, pamoja na mashahidi wengine ili kukamilisha upelelezi wajinsi kodi na ushuru ilivyokwepwa kupitia bandarina ICD’s

from Blogger http://ift.tt/1Pl7UwS
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/1JvXPJ2

No comments:

Post a Comment