Akizungumza na waandishi wa habari jana, kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Wibroad Mtafungwa alisema kuwa Novemba, 10 bibi huyo awali ilidaiwa amepote ambapo jeshi la polisi likishirikiana na wakazi wa kijiji cha Igominyi walimtafuta bibi huyo kwa siku kadha bila mafanikio.
Alisema kuwa taarifa za kupatikana na kwa bibi huyo katika shimo la choo zilifika ofisini kwake na kumkuta bibi huyo akiwa fukiwa katika shimo hilo na uchunguzi wa daktari ukionyesha alinyonhwa, uchunguzi wao umefanya kuwakamata watu watatu wa familia moja na mtommoja mfanyakazi wa ndani wa bibi huyo.
Mtafungwa aliwataja wahusika wa tukio hilo kuwa ni Zawadi Mlowe,(32), ambaye alikuwa mfanyakazi wa ndani wa pili ni Longinusi Mbulikwe(40, Neema Hongoli Hedimelik Mkongwa wote wakiwa wakazi wa Limage.
Alisema kuwa bibi hiyo alipotea tangu Novemba 10 mwaka huu ambapo jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kwaajili ya kuwapandisha mahakamani.
Alitaja chanzo cha mauaji ya bibi huo ni mgogoro wa ardhi ambapo ndugu wa marehemu walikuwa na tama ya mashamba yake ambayo yanarutuba.
Alisema kuwa jeshi hilo likikamilisha uchunguzi wake litawapandisha mahakamani washitakiwa hao kutokana na kosa la mauaji ya kukusudia.
from Blogger http://ift.tt/1NZG7mT
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/1X52W9c
No comments:
Post a Comment