Taarifa zilizotufikia hivi punde katika chumba chetu cha habari, Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila (pichani) amepata ajali na kufariki dunia alfajiri ya leo eneo la Msolwa-Chalinze.
Elimtaa Blog inaungana na wanachama wa DP pamoja na watanzania wote katika kuomboleza kifo cha Mchungaji Mtikila, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Mchungaji Mtikila Amen.
Pichani ni gari iliyopinduka na kumuua Mchungaji Mtikila.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama cha DP, Abdul Mluya.
Elimtaa Media inaendelea kukusanya taarifa zaidi na tutawajuza wasomaji wetu hapo baadae.
By MoDewijBlog
from Blogger http://ift.tt/1KT7FHE
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/1L6MJK6
No comments:
Post a Comment