VITENDO vya Rushwa maneno machafu kwa baadhi wa watumishi wa hospitali wakiwemo wauguzi na madaktari vimedaiwa kuwa ni hulka ya mtu binafsi na sio maadili wanayofundishwa katika vyuo vya taaluma yao.
Hayo yamebainishwa na baadhi ya wanachuo na wahitimu wa chuo ya Sayansi ya afya Bulongwa cha wilayani Makete Mkoani Njombe, ambao wamesema kuwa vitendo vya Rushwa na Lugha chafu havifundishi chuoni na kuwa wanafundishwa kuwa wataratibu wanapo hudumia wagonjwa.
Mmoja wa wahitimu katika chou hicho Dr. Daniel Ngailo amesema kuwa miaka ya sasa maadili ya taaluma hiyo wamekuwa wakifundishwa na kuwa ndio maana katika vituo vya afya mpaka hospitali vitendo vya maneno machafu vimepungua kutokana na maadili kufundishwa sana.
Hata hivyo Maulisia Mlowe anaye hitimu mafunzo ya uuguzi anasema kuwa vitendo vya rushwa na kashifa kwa wagonywa vinakuwa ni hulka ya mtu binafsi na tamaa huku akisema kuwa serikali iongeze kiwango cha mishahara ili kuhakikisha kuwa wauguzi wanafanya kazi bila kuwa na tamaa ya pesa kutoka kwa magonjwa na kuondoa vitendo vya Rushwa.
Kwa upande wake mkuu wa chuo cha Bulongwa, John Matala amesema kuwa serikali imekuwa ikiwatembelea mara kwa mara na kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa inakuwa bora na kuwa katika chuo hicho wahitimu wanao toka wanaende kuwa wenye maadili kutokana na walivyo wafundisha.
Alisema kuwa chuo hicho wanamalengo ya kuwa chuo kikuu na kuanza kutoa elimu ya afya kwa hadhi ya chuo kikuu, na kuwa wanatarajia kuongeza vitengo vingine vya kutoa wahudumu wa afya.
Naye mgeni rasimi katika maafari hayo aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Songea kwa sasa ni mgombea wa ubunge jimbo la Makete Prof. Norman Sigalla amesema kuwa chuo hicho kinatakiwa kuwa na wakuu wa bodi wenye uwezo wa kifedha na watu wenye ubunifu ili chuo hicho kufikia malengo yake kwa haraka ya kuwa chuo kikuu.
Alisema kuwa kuna watu wenyeuwezo ka kuandaa miradi katika wilaya hiyo na chuo kinatakiwa kuwatumia watu hao ili kiweze kufikia malengo yake mapemba ya kuwa chuo kikuu ya afya kama yalivyo malengo yao.
from Blogger http://ift.tt/1LeP6La
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/1Org2dO
No comments:
Post a Comment