Saturday 29 August 2015

RAIS KIKWETE AZINDUA KAMPENI YA MAMA ONGEA NA MWANAO

Wasanii wa Filamu nchini Wema Sepetu na Steven Nyerere wakimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. Jakaya Kikwete katika Hoteli ya Hyatta Kempinski jijini Dar es Salaam kuzindua kampeni ya ‘Mama Ongea na Mwanao’ ili aipigie kura CCM. Kampeni hiyo imeratibiwa na wasanii wa filamu wakiongozwa Wema Sepetu na Steven Nyerere.


 Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. Jakaya Kikwete, Waziri wa Sheria na Katiba ambaye pia ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusaino wa Kimataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Paul Makonda (kushoto) wakiwa na wenyeji wao Wema Sepetu na Steven Nyerere katika uzinduzi wa kampeni ya ‘Mama Ongea na  Mwanao’ ili aipigie kura CCM. Kampeni hiyo imeratibiwa na wasanii wa  filamu jijii Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. Jakaya Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa kampeni hiyo.
Msanii wa Filamu, Wema Sepetu akimkabidhi Rais Dkt. Jakaya Kikwete tuzo maalum kwa kutambua mchango wake katika kulinda na kuthamini kazi za wasanii nchini ambapo katika kipindi chake cha uongozi wamepata manufaa makubwa. Wema alikabidhi tuzo hiyo kwa niaba ya baadhi wasanii wa filamu na muziki nchini wanaoshiriki katika kampeni ya ‘Mama Ongea na Mwanao’ yenye lengo la kuwahimiza wanawake kuwahimiza watu kuipigia kura CCM kwa kuwachagua wagombea wake katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
(Picha na Freddy Maro)

from Blogger http://ift.tt/1NOf5hz
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/1ErZX7E

No comments:

Post a Comment