Saturday, 18 March 2017

AFYA: FAIDA 6 ZA KUOGA KWA KUTUMIA MAJI YA MOTO

Watu wengi hupendelea kutumia maji ya moto kuoga pale hali ya hewa inapobadilika na kuwa ya baridi au wakati mwingine mtu anaumwa hivyo anatumia maji ya moto.

Sehemu kama Dar es Salaam ni mara chache utakuta wakazi wake wanaogea maji ya moto kutokana na hali ya joto katika jiji hilo.

Lakini kwa ajili ya urembo na afya ya ngozi, maji ya moto yanatajwa kuwa ni kitu muhimu sana kama vilivyo vipodozi vingine vinavyoisaida ngozi yako kuwa nyororo.
Gazeti la Mwananchi limeandika baadhi ya faida zitokanazo na matumizi ya maji  ya moto angalau mara tatu kwa wiki
1. Kulainisha na kutunza ngozi
Maji ya moto husaidia kulainisha ngozi yako tofauti na ukitumia maji ya baridi. Maji ya moto hasa yaliyo katika jakuzi ambapo utatumia muda mrefu kidogo ngozi yako ikiwa kwenye maji, husaidia kuilainisha ngozi yako na kuiweka katika hali nzuri.
2. Usingizi
Kama huwa unapata matatizo kupata usingizi usiku, amka oga kwa kutumia maji ya moto kwani husaidia kulainisha misuli ya mwili wako na itakaa sawa na utaweza kupata usingizi.
3. Kukuweka katika hali nzuri
Kuna wakati mwingine mtu hujisikia uchovu wa mwili na kutotaka kufanya chochote (Off mood). Ukioga kwa maji ya moto yatakusaida kukuondolea uchovu na utajisikia mwenye nguvu na upo tayari kukabiliana na changamoto za siku.
4. Kuchangamsha ubongo
Unapooga kwa kutumia maji ya  moto husaidia kuchangamsha ubongo na kuufanya uweze kufanyakazi kwa ufanisi na kwa haraka zaidi.
5. Kushusha shinikizo la damu
Ukiachanna na masuala ya urembo, kuoga maji ya moto kunatajwa kuwa ni njia ya haraka ya kusaidia kushusha shinikizo la damu. Tafiti zinaonyesha kuwa mtu mwenye shinikizo la damu la kupanda, akioga kwa maji ya moto husaidia kushusha.
6. Kusaidia mzunguko wa damu
Ukioga kwa kutumia maji ya moto husaidia kusisimu na kuitanua mishipa ya damu hivyo kuwezesha damu kuwa na mzunguko mzuri mwilini.
Licha ya kuwa maji ya moto ni mazuri kiafya, unashauriwa kuto oga kwa maji ya  moto sana kwani huathiri ngozi.

from Blogger http://ift.tt/2m9rhUJ
via IFTTT

from WordPress http://ift.tt/2nuHZ0Y
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2mCfGtf
via IFTTT

from WordPress http://ift.tt/2mzqPdS
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2mQjOab
via IFTTT

from WordPress http://ift.tt/2mawJqf
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2mQOmbI
via IFTTT

from WordPress http://ift.tt/2maQY7b
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2mR70jR
via IFTTT

from WordPress http://ift.tt/2mbvWpc
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2mRP3BM
via IFTTT

from WordPress http://ift.tt/2mbKh51
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2mcmpOz
via IFTTT

from WordPress http://ift.tt/2n7tX4e
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2nxOO1X
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2mCPoGx

No comments:

Post a Comment