Sunday 19 February 2017

Zitto: Manji Anakomolewa, Sasa Anyang’anywa Hisa Zake za Tigo na Serikali..!!

Yanayoendelea dhidi ya Yusuf Manji yanashabikiwa na baadhi yetu kwa sababu wanadhani hayatawafika. Tabia ya kukomoa mtu ni tabia mbaya na ina madhara makubwa katika nchi. Ni dhahiri kuwa Manji sasa anaonewa na kudhalilishwa ili kumkomoa kwa sababu ambazo watawala wanazijua wenyewe. 
Wakati suala la kutumia unga lipo kortini, Serikali imeamua kumnyanganya hisa zake za Tigo. Sio kwamba Serikali itachukua hisa Hizo, la hasha. Ila Manji azikose tu. Unajiuliza, Serikali hii hii imeacha matapeli wa PAP kuitwaa IPTL na TANESCO inawalipa zaidi ya tshs 300m kila siku. Leo mpaka mahakama inatumia suo moto kurudisha suala la hisa za Manji kwenye Tigo ambalo halina maslahi yeyote ya Taifa. Kwanini Mahakama haikufanya suo moto kurudisha fedha za Tegeta Escrow? 
Watanzania wajue tu kuwa, mwaka 2004 Serikali iliachia hisa zake 20% kwenye Tigo kwa USD 750,000 ( vichekesho) kwa kuiuzia kampuni kutoka Luxembourg. Badala ya Serikali kuhangaika na maafisa wake walioachia hisa kutoka nje ya Tanzania wanahangaika na Mtanzania aliyezirudisha hisa Tanzania. 
Uhamiaji wanamwita kuhusu wafanyakazi wake wageni kana kwamba yeye Yusuf ni Afisa Rasilimali watu wa kampuni. Aliko Dangote hakuitwa uhamiaji kwa suala la wafanyakazi wake ila Manji anaitwa. 
Wakifanikiwa kwa Manji atatafutwa mwengine, Ni sawa na kula nyama ya mtu. Hutaacha. 
Manji anaweza kuwa ana madudu mengi Sana, ahukumiwe kwa haki kwa makosa yake. Asikomeshwe kwani ukomeshaji hautaishia kwake. Asionewe. Atendewe haki. 
Anyways Kama Mwana Simba, nawasihi Yanga achaneni na mambo ya mabango uwanjani. Hayasaidii lolote.

from Blogger http://ift.tt/2l9giby
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2lyMGpn

No comments:

Post a Comment