JESHI la polisi mkoani Mbeya linawashirikiria watu 11 kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa Kopyuta 12 mali ya chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Mbeya kilicho eneo la Sokomatola jijini hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,Dhairi Kidavashari alisema kuwa watu hao wamekamatwa na vitu hivyo Februali 15 mwaka hu katika mkazi yao baada ya jeshi hilo kufanya msako.
Kamanda Kidavashari alisema mbali na Kompyuta hizo watu pia watu hao walikutwa na Monita mali ya chuo hicho ambazi zilikuwa zinatumika kufundishia chuo hapo.
Alisema baada ya kuhojiwa watuhumiwa walikiri kuhusika na matukio ya kuvunja Ofisi za Chuo majira ya Usiku na kuiba vifaa hivyo ikiwa ni pamoja na kununua vifaa vya wizi.
Alisema kuwa katika msako hao Jeshi hilo lilikamata Komyuta 15 kati ya hizo 11 ni mali ya chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Mbeya.
Aidha katika hatua nyingine Jeshi hilo linawashikilia watu 39 wa tuhuma za kujihiusisha na matumizi ya dawa za kulevya kati yao 33 wabiwa ‘Unga” na wauzaji 6.
Kamanda Kidavashari alisema kuwa dawa zilizo kamatwa ni pamoja na
Bangi,kilogramu 18, baada ya kuendesha msako mkali katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya.
Aidha jeshili hilo limewatia mbaroni watu wengine nane baada ya kukutwa na pombe haramu ya Moshi ya ‘gongo” lita 53 pamoja na mitambo ya kutengenezea pombe hiyo.
from Blogger http://ift.tt/2lgQbxK
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2m6Z6RY
No comments:
Post a Comment