Tuesday, 21 February 2017

Mahakama yamhukumu aliyeiba Kanzu Msikitini akafyeke nyasi

MWANAMUME aliyekiri shtaka la kuiba kanzu yenye thamani ya Sh5,000 katika msikiti wa Jamia wiki iliyopita aliamriwa afanye kazi ya kufagia na kukata nyasi katika afisi ya chifu nchini Kenya
Joshua Lukanda Bukenya aliomba msamaha kortini na “kuapa hatarudia kufanya kosa hilo siku nyingine.”
Alieleza korti kwamba alikamatwa na mwenye kanzu hiyo Bw Ahmed Abdullahi akipeleka kwa askari wanaolinda msikiti.
“Naomba msamaha niliiba kutoka mahala pa kuabudia. Nilikamatwa na mwenye Kanzu hiyo kabla ya kuipeleka kwa Askari wanaolinda msikiti huu wa Jamia ulioko kati kati mwa jiji la Nairobi,” Bukenya alisema.
Bw Bukenya aliyejawa na haya alipoulizwa na hakimu sababu ya kuiba msikitini alisema “kwa kweli nimeghairi matendo yangu. Naungama kosa hili mbele ya hii mahakama nakuahidi kwamba sitawahi lirudia tena. 
Naomba nisamehewe.”
Hakimu mkuu katika mahakama ya Milimani Nairobi Bw Francis Andayi alimwuliza mshtakiwa sababu ya kuiba kanzu hiyo na hata akakubali kufikishwa kortini badala ya kumwomba mwenye msamaha na kumrudishia kanzu hiyo.
“Mbona unataka kujaza hii korti na kesi ambayo ungeliomba msamaha na hata ungelifikishwa kortini,.” Bw Andayi alimwuliza mshtakiwa.
Akaendelea kumweleza , “Ningelikuwa wewe ningeliomba msamaha kisha niombe niachiliwe.”
Aliongeza kumweleza “hata ukikiri na uombe msamaha hii mahakama itakufunga siku moja au mbili kufanya kazi katika afisi ya chifu ndipo usirudie kufanya makosa kama hayo tena.”
Mshtakiwa alipokea ushauri wa hakimu na kuomba msamaha.
Alifungwa kifungo cha kufanya kazi kwa afisi ya chifu kwa muda wa wiki moja na kuonywa asirudie kosa hilo tena.
Alikiri aliiba kanzu hiyo mnamo Februari 17, 2017.
Chanzo: swahilihub

from Blogger http://ift.tt/2m7dUka
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2m7hSJD

No comments:

Post a Comment