Unaukumbuka ule mkasa wa Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kubadilishana jezi ya timu ya taifa na mshambuliaji wa Cameroon Samuel Eto’o? Nakusogezea Cannavaro alivyoelezea stori nzima namna tukio lilivyokuwa.
Cannavaro amesema, alikuwa anajua kabisa kuwa, timu ilikuwa na uhaba wa jezi na wachezaji walikuwa hawaruhusiwi kubadilishana jezi, baada ya mechi jezi zilikuwa zinakusanywa na kurudishwa kwa ajili ya kufuliwa na huenda zingetumika tena kwenye mchezo mwingine.
Lakini yeye aliamua kubadilishana jezi na Eto’o kwa sababu nyota huyo wakati huo alikuwa kwenye kiwango bora sana na alikuwa maarufu kutokana na kucheza Barcelona na isitoshe Eto’o mwenyewe ndiye aliyeomba kubadilishana jezi na Cannavaro
“Kipindi hicho tulikuwa na uhaba wa jezi kwenye timu yetu ya taifa na tulikuwa haturuhusiwi kubadilisha jezi kutokana na uhaba wa jezi katika timu.”
“Ila ile mechi ambayo tulicheza na Cameroon nyumbani kwao, tulicheza vizuri sana nakumbuka nilicheza na Said Swed Kusi kama mabeki wa kati nilicheza vizuri sana na tuliwamudu kuanzia dakika ya kwanza hadi ya 90.”
“Baada ya mechi kumalizika, nikawa nimekaa chini nalia kwa sababu walitufunga goli lao la ushindi dakika za mwishoni, Eto’o akaja akanipa mkono akaniomba tubadilishane jezi wakati huo alikuwa moto anacheza Barcelona, japo tulikuwa na uhaba wa jezi unaanzia wapi kukataa kubadilishana jezi na Eto’o?”
“Nikatoa jezi huku najua kutakuwa na matatizo, nikaona huyu ni mtu mkubwa nikatoa jezi na yeye akanipa yake, baada ya pale hatukuwahi kuwasiliana tena.”
“Sasa balaa likaanza tulipoingia kwenye basi tunatoka uwanjani kurudi kambini tulipofikia, baadhi ya wachezaji wakawa wanasema sisi haturudishi jezi kama mnataka turudishe mwambieni Cannavaro arudishe jezi yake, baadae meneja akanifata akaniambia itabidi ukatwe hela kufidia ile jezi. Nakumbuka nilikatwa kama shilingi 60,000 au 70,000 lakini kwangu mimi ilikuwa poa tu wala sikukasirika.”
“Baadae wazanzibar wakaanza kusema wanataka wachange hiyo pesa kwa nini nikatwe kwa sababu ya kubadilishana jezi, lakini mwisho wa siku kila kitu kilikuwa sawa.”
“Kuanzia hapo utaratibu ukabalika, Tenga wakati huo akiwa rais wa TFF akasema, mtu akicheza jezi inakuwa mali yake hiyo ikasaidia hadi leo watu wanauwezo wa kubadilishana jezi lakini hayo yote yalikuja baada ya lile tukio langu na Eto’o.”
“Ile jezi bado ninayo hadi leo, ni kumbukumbu kwangu huwa siivai nimeiweka tu kwa sababu ya familia yangu, watoto wakikua siku moja nitawaelezea tukio zima lilivyokuwa.
from Blogger http://ift.tt/2kVohXs
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2kVxrTu
No comments:
Post a Comment