TAASISI ya kupambana na rushwa Tanzania imesema kuwa katIka kipindi hiki cha uchaguzi matukio ya rushwa kutikaka na kutumia muda mtegu kuwekeza katika kuelimisha jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa takukuru mkowa wa Njombe, Charles Nakembetwa amesema kuwa walijikita katika elimu kwa wananchi kuhusiana na viashiria vya rushwa na kuifanya kazi yao kuwa nyepesi.
Amesema kuwa katika kipindi hiki cha uchaguzi taasisi hiyo imefanya kazi kwa urahisi kutokana na jamii kuelewa rushwa ninini na kutoa taarifa kabla ya kutokea kwa rushwa.
Nakembetwa amesema kuwa licha ya baadhi ya wanajami kuendeleza vitendo hivyo lakini jamii imekuwa ikitoa taarifa mapema na kudhibiti uharifu huo kabla haujatokea.
Amesema kuwa kwa maka huu kuna matukio ambayo wapo katika uchunguzi wake ili kuyapeleka mahakamani na kuwa yakikamilika na kupata ushahidi wa kutosha watayafikisha mahakamani.
Hata hivyo amesema kuwa kazi yao kwa mwaka huu ilikuwa ni rahisi kutokana na kuwa namsingi mzuri a kutoa elimu na wananchi kuwapa taarifa wannapoona viashiria.
from Blogger http://ift.tt/1KTnvP2
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/1N8GNle
No comments:
Post a Comment