Tuesday 27 October 2015

MATOKEO YA UCHAGIZI MAJIMBO MAWILI MKOA WA NJOMBE

CHAMA cha mapinduzi jimbo la Lupembe kimetangazwa mshidi kwa kishindo katika uchaguzi wa ubunge, Urais na udiwani uliofanyika jumapili hii, huku ngombea wake Joram Hongoli kura 20430 tofauti na Edwin Swale akipata kura 10407, wa chadema.

Elimtaa wanarpoti

Matokea hayo yametangazwa na mkurugezi wa halmshauri ya wilaya ya Njombe Paulo Malala, ambaye Ndio msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, ambalo vyama viliwili vilisimamisha wagombea wa ubunge.

Akitangaza matokeo hayo bila kutaja kata ngapi zimeenda kwa chama gani Malala alisema kuwa jimbo hilo matokeo katika jimbo lote tayari yamesha bandikwa ka kata zote na kuwa matokeo ya urais yametumwa tume ya uchaguzi.

Alisema kuwa jimbo la Lupembe uchaguzi uliendeshwa kwa amani na utulivu huku katika majumusisho ya kura za madiwani ulikamilika majira ya saa 10 ya usiku na kwa majumuisho ya kura za ubunge kukamilika majira ya saa 8 mchana.

Alisema mgombea wa ubunge wa jimbo la Lupembe aliyeshinda ni kutoka chama cha Mapinduzi CCM, Hongori amepata kura 20430  na mgombea wa chama cha demokrasia na maendeleo Swale amepata kura 10407.

Aidha katika jimbo la Njombe kusini kuna wabunge waliokuwa wamesimama kusaka nafasi hiyo ni kutoka katika vyama vitatu vya Chadema, Act-Wazalendo na CCM.

Katika jimbo hilo mbunge aliyeshinda ni kutoka chama cha CCM, ambaye ni Edward Mwalongo Kwa kupata kura 27285 na aliye fuatia ni Emanuel Masonga kutoka chama cha Chadema aliyepata kura 23003, Mgombea wa chama cha ACT Wazalendo, Emilian Msigwa amepata kura 3888 na mgombea wa chama cha DP, Wiliam Myegeta akiambulia kura 94 huku katika jimbo hilo kulikuwa na kata 13.

Katika jimbo hili kata 8 Zimeenda kwa chama cha CCM, na kata tano zikienda upinzani kwa chama cha Chadema.

Huku katika jimbo la Ludewa mkoani hapa lililopigwa kura za uduwani na urais pekee lina kata 25 huku kata 24 zikitwaliwa na CCM na kata moja kwenda katika chama cha demokrasia na maendeleo kata hiyo ni ya Madilu.

Katika majimbo mengine ya mkoa wa njombe matokeo yake mpaka jana jioni matokeo yake yalikuwa bado kuwa wazi.

from Blogger http://ift.tt/1kK6DFe
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/1jN0uIh

No comments:

Post a Comment