Friday, 28 August 2015

VOA yaanda Kongamano juu ya Mitandao ya Kijamii na Uchaguzi Tanzania


Washiriki katika Kongamano la VOA , mjini Dar Es salaam

Washiriki katika Kongamano la VOA , mjini Dar Es salaamSauti ya Amerika VOA inaendesha  kongamano la changamoto za mitandao ya kijamii katika utangazaji mjini Dar es Salaam, katika hoteli ya Serena.

Kongamano hilo linahudhuriwa na wajumbe wa  redio washirika wa VOA huko Tanzania kujadili jukumu la mitandao ya kijamii katika uchaguzi mkuu na jukumu lao katika kuwaelimisha wapiga kura.
Kongamano litafuatiwa na mkutano maalum na redio washirika kujadili namna ya kushirikiana zaidi katika siku zijazo. Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, VOA, Negussi Mengesha pamoja na Mwamoyo Hamza mkuu wa Idhaa ya Kiswahili na Steve Ferri, mkuu wa kitengo cha Teknohama, ni miongoni mwa wanaohudhuria kongamano hilo.

from Blogger http://ift.tt/1JpGxPL
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/1JAG8GW

No comments:

Post a Comment